Baixar aplicativo
98.77% Tafadhali, Nipende(Please, Love me) / Chapter 242: HUYU MWANAMKE

Capítulo 242: HUYU MWANAMKE

Mpendwa Msomaji wangu,

Ni muda umepita pasipo kuweka mwendelezo wa simulizi hii. Nisamehe sababu mambo mazito yalinitinga. Sasa nakukaribisha tena kuweza kuendelea pale tulipoishia. Nitaendelea kuweka walau sura moja kila siku ili tukimbilie hitimisho. Simulizi yangu mpya ya Lucinda nimeanza kuipa sura kabla hatujaendelea nayo hapa.

Karibu usome

***************

Linus baada ya kuingia chumbani kwake, alijitupia kitandani huku tabasamu harufu likionekana usoni. Maneno ya Derrick yalianza kurudia kichwani kwake..

"Bro naona ukaribu wako na Beruya umepamba moto"

Akakumbuka na maneno aliyoambiwa na Allan, akacheka taratibu na kuinuka huku akifungua vifungo vya shati

"Hivi naonesha mabadiliko au wanajaribu kunishawishi" akawaza

Akapita hatua kuelekea bafuni lakini mlio wa simu ukamshtua, akaichukua pale kitandani, "Allan"

"Hello comrade" akapokea

"Comrade nina dharura na naomba msaada wako wa haraka" sauti ya Allan ilisikika masikioni kwa Li na mara moja akatambua alikuwa kwenye gari iliyokuwa ikienda kasi

"Niambie cha kufanya" akaitika

"Nakuja hapo mara moja niko na mtu"

"Hakuna shida hapa ni nyumbani comrade" Li akamwambia

"Asante kaka" Allan akakata simu na kumuacha Li akiwaza ni dharura gani iliyompata

*************

"Una wasi wasi wa bure hawawezi kutupata ngoja tuingie mjini" Renatha akamwambia Allan baada tu ya kukata simu

"Renatha hatujui tumechokoza aina gani ya watu tukienda kwako tutakuwa tumewaonesha unapoishi na __"

"Allan, hawataweza kuiona hii gari tukiingia mjini hata sasa wako mbali sana kama wanatufuatilia, usiogope"

Kwa namna Renatha alikuwa akipishana na magari na kuyapita, Allan alimtazama huku akitamani kutabasamu lakini alihisi sio muda sahihi..

"Una muda gani tangu uanze kuendesha gari!" Allan uvumilivu ukamshinda akaona aulize

Renatha akageuka kwa haraka na kumwangalia Allan huku atabasamu likiwa usoni

"Tangu nikiwa na miaka 10, usiniulize ilikuwaje katika umri huo mdogo"

Allan akanyamaza kimya akageuka nyuma kuangalia kama kulikuwa na dalili ya gari inayowafuatilia nyuma lakini hakuona isipokuwa lori lilionekana kuwa katika safari zake.

**************

Baada ya Renatha kushuka kwenye usafiri wa pikipiki ambao aliuchukua mara alipoachana na Allan. Aliamua hivi japokuwa Allan alisisitiza aende nae kwa Li lakini alikataa. Hakutaka pia kuonekana ameongozana na Allan, jambo ambalo lilimpa ukakasi kulielewa.

"Allan tafadhali hebu tusibishane ni kwa faida yako. Nashuka hapa na tafadhali usishuke."

Allan akamuangalia aliposhuka, kisha akatembea hatua chache kabla ya pikipiki aliyoiagiza kumchukua, haijasimama miguuni pake. Renatha akapanda pasipo kugeuka nyuma. Allan akaendesha akiwafuatilia kwa nyuma huku mara kadhaa akikaribia kuwapoteza.

Aliposhuka Allan alikuwa hatua chache kutoka aliposimama, akaendesha gari kwa mwendo wa pole pole akimfuatilia hadi alipofika kwenye mlango wa kuingia.

Renatha hakugeuka nyuma japokuwa alitambua kuwa Allan alikuwa akimfuatilia huku taa za gari akiwa amezima.

Baada ya kumuona ameingia, Allan akaondoka maeneo yale kwa haraka akaelekea kwa Li.

"Nini kinaendelea comrade maana umenishtua sana" Li akamwambia Allan mara walipoingia ofisini kwa Ed ili waweza kuwa na faragha ya mazungumzo

"Li, niko matatizoni, naongeza tatizo juu ya tatizo" Allan akasema, kisha akamsimulia mkasa wote uliowakuta na Renatha.

"Kweli unampenda huyu mwanamke" Li akamwambia baada ya kumsikiliza..

"Sijui itakuwaje rafiki yangu! Naomba unisaidie Captain asiendelee zaidi na uchunguzi hadi nipate ukweli wa Renatha!"

"Siwezi kukuhakikishia hilo, maana unamjua Captain na Bro, ila nitajitahidi" Li akamwambia, "Unadhani Renatha anaficha kitu gani?"

Allan akamuangalia Li kisha akainama "Hata sielewi lakini ninahisi ni kama analazimishwa kufanya hivyo"

"Mtu mzima kama yule analazimishwaje comrade!" Li akatikisa kichwa huku akiinua nyusi

"Li naomba unisaidie najua sio kitu chepesi, naamini nitapata majibu hivi karibuni" sauti ya Allan sasa ilionesha kabisa kumsihi Li..

"Sawa. Unaweza ukapumzika hapa hadi kutakapokucha"Li akamwambia huku akiinuka

"Asante sana comrade hata hivyo naomba niende nyumbani, tuonane kesho" Allan akamuaga

Wakatoka nje na kisha wakaagana.

"Tafadhali karibu kupumzika na utafakari kwa kina" maneno ya Li kwa Allan mara alipoingia kwenye gari ili kuondoka.

"Nitafanya hivyo comrade"

Li akabaki amesimama akitazama gari iliyotoka na mara mlinzi alipofunga geti akashusha pumzi

"Mapenzi haya mh"


Load failed, please RETRY

Status de energia semanal

Rank -- Ranking de Poder
Stone -- Pedra de Poder

Capítulos de desbloqueio em lote

Índice

Opções de exibição

Fundo

Fonte

Tamanho

Comentários do capítulo

Escreva uma avaliação Status de leitura: C242
Falha ao postar. Tente novamente
  • Qualidade de Escrita
  • Estabilidade das atualizações
  • Desenvolvimento de Histórias
  • Design de Personagens
  • Antecedentes do mundo

O escore total 0.0

Resenha postada com sucesso! Leia mais resenhas
Vote com Power Stone
Rank NO.-- Ranking de Potência
Stone -- Pedra de Poder
Denunciar conteúdo impróprio
Dica de erro

Denunciar abuso

Comentários do parágrafo

Login