Akaamua na kumuongezea juisi, kitendo ambacho kilimfanya Aretha kuinama huku 'asante' ikimtoka kinywani.
Ed alijisikia vyema kuona walau mgeni wake anajisikia vyema. Akarudi kukaa kwenye kochi lake akimtazama Aretha ambaye wakati huu alitafuna biskuti na kunywa juisi kwa uso wa furaha.
Akajikuta moyoni akimshukuru sana Allan kwa kuwa na uchaguzi bora, asijue Allan alimuuliza Loy aina gani ya biskuti anapenda. Ha ha ha
"Aretha" aliita Ed
"Eehhhm" akaitikia Aretha ambaye alionekana kufurahia biskuti zile na juisi.
"Nini kilikusukuma kuniuliza maswali yale" Ed aliuliza huku akimkazia macho Aretha ambaye wakati huu alimeza biskuti aliyokuwa akitafuna na kumwangalia
"Maswali uliyoniuliza ni kama uliwahi kuyaona maisha yangu yanapungukiwa" aliendelea Ed
"Aaaa ahm hapana sio hivyo" alitikisa kichwa kupingana na alichokisema
"Niambie Aretha" alisema Ed na kuegama kwenye kochi huku akipandisha mguu mmoja juu ya mwingine
Aretha alihisi kukamatwa maana hakuwa mzuri kwenye kujieleza. Akaweka boksi la biskuti mezani kisha akaanza kwa kigugumizi
"Ma..aahm..mama aliwahi kuniambia kuwa mara nyingi....aah... watu huwaona matajiri kama wenye kila kitu lakini wanaweza kuwa watu wasio na furaha sababu ya huo utajiri"
"Unadhani mimi naweza mmoja wa hao watu?" aliuliza tena Ed huku akizidi kuangalia uso wa Aretha kuzisoma hisia zake.
Aretha akarudisha tena macho yake kwenye vidole vyake na kisha kwa huzuni akasema
"Sijui kama na wewe hauna furaha, lakini natamani uwe na furaha na uishi maisha yako kwa amani"
Ed sasa moyo wake uliyeyuka kama barafu lakini hakuacha kuendelea kutaka kujua
..
"Kwa nini unatamani hivyo?" Aliuliza tena
Aretha aliinua uso wake na kumfanya Ed kuiona huzuni iliyoonekana wazi usoni kwa binti huyu...
"Aaahm basi tu, ninapenda tu unavyojitoa kwa jamii natamani wakati jamii inafurahi nawe ufurahi"
Kuna namna Ed alihisi, japokuwa bado alifikiri kuna kitu Aretha anajaribu kukificha, bado aliguswa na hisia zile.
Kama kweli ananiwazia hivi basi anaweza kuwa binti mwema. Aliwaza Ed ambaye aliinuka na kuchukua chupa ya maji.
Aretha aliinua macho yake kumfuatilia Ed, alipoona akirudi akachukua biskuti na kuendelea kula akiangalia kwingine na sio usoni kwa Ed.
"Kujibu swali la pili, nikuulize kitu?" Ed alisema huku akitabasamu
"Aaahmm....sawa" alijibu Aretha huku akibugia funda la juisi.
"Unaweza kumtania mtu?" Aliuliza Ed
"Ha ha ha naweza japokuwa sio sana" alijibu Aretha na kumfanya Ed kujua hilo lilikuwa jibu la ukweli akaendelea
"Unaweza kunifanya nicheke?" aliuliza Ed kwa shauku kuona Aretha anachoweza kufanya..
"Kukuchekesha aah... sidhani labda nikikuzoea" alimwambia kisha nae kamtupia swali Ed..
"Huwa unapata muda wa kucheka na kufurahi na wengine?"
"aaamh... yes, nikiwa na familia mara chache napopata nafasi" alijibu Ed.
Aretha akamwangalia Ed kwa sekunde chache kisha akarudi kufinya vidole vyake akasema taratibu
"Uwe unacheka mara nyingi zaidi, it's good to laugh"
Kimya cha muda mfupi kikapita, Ed akitafakari alichosema na mwishowe akamwambia
"Sawa nitafanya hivyo, asante kushauri"
Ghafla tabasamu lilionekana kwenye uso wa Aretha na akamuonesha alama ya dole gumba juu kuonesha amefurahi.
Subiri nini kimemfurahisha, alijiuliza Ed. Yaani anatamani niwe na furaha, kwani anahisi huwa sicheki. Kuna kitu kimefichika kwa huyu binti. Ed alikuna kidevu chake na kumuangalia Aretha kisha akauliza
"Nini unapenda kufanya usipokuwa chuoni?"
"Eh. . Kuchora" alijibu
"Naweza kuona picha unazochora?" Aliuliza Ed
Macho ya Aretha yakawaka kwa mshangao
"Utapata muda?" Akauliza Aretha
"Nitapata kama nilivyopata huu wa leo?" Alijibu Ed akiachia tabasamu ambalo lilimfanya Aretha apotee katika ulimwengu wa mawazo yake hadi aliposhtuliwa
"Aehhhm" alikohoa Ed
"Sawa nitakuletea siku nyingine" alijibu Aretha
"Umeahidi?" Aliuliza Ed.
Tabasamu laini kutoka kwa Aretha likampa hakikisho.
"Nafikiri niondoke sasa" akasema Aretha huku akiinua begi lake tayari kutoka.
"Oooh, basi sawa. Asante kuja kunitembelea" akashukuru Ed
"Nimefurahi kuja hapa, asante kwa juisi na my favourate biskuti"