App herunterladen
100% CHOZI LA UNYONGE / Chapter 12: SURA YA KUMI NA MBILI

Kapitel 12: SURA YA KUMI NA MBILI

Sir, I am suggesting that we don't tell her about her parents," Labibu alisikia sauti kwa mbali kutoka pale alipolazwa.

"Ni heri tumjuze mapema kwa sababu hata akiinuka happy alipo, hilo ndilo litakuwa swali la kwanza," alisikia sauti ya pili ikipinga ya kwanza, "tutamfahamisha lakini hatutaruhusu aondoke."

Labibu aliinua kichwa kutoka kitandani na kufumbua macho, alikuwa amefungwa bendeji kichwani, alijaribu kupindua shingo kukagua alipokuwa lakini akahisi maumivu. Alishangaa zaidi kujipata kwenye kitanda hospitali. Alijaribu kuvuta kumbukizi zake mpaka pale alipokuwa lakini akashindwa, aliinuka polepole akaelekea dirishani, akavuta pazia upande mmoja kupenyeza ndani miale ya jua.

"Shikamoo dadangu," alisikia sauti ikimsalimu kutoka nyuma.

"Marahaba," Labibu aliitikia salamu akigeuka, "naitwa Labibu."

"Nami naitwa doc Jack," mwenzake alijitambulisha, "nimefirshi kukuona katika hali hii tena."

"Unaweza kunieleza kilichotokea doc," Labibu alimsihi, "nimejaribu kukumbuka nilivyofika hapa lakini..."

Daktari aliangalia chini baada ya Labibu kumuuliza, alikumbuka jinsi siku hiyo waliyompata ilikuwa ya kutatanisha kwa upande wake.

Kwanza ilianza kwa kusababisha kifo cha mama mjamzito kwa sababu ya upungufu wa vifaa na dawa za kujifungua katika hospitali hiyo. Saa tano za usiku akiwa bado anaomboleza kilichotokea, simu ikapigwa kutoka kituo cha polisi ikiwataka wafike kwa daraja la Maomboleza kwa haraka.

Bila kupoteza wakati, alimjuza muuguzi aliyekuwa kwenye masjala kisha wakaingia gari la wagonjwa na kuondoka, walipofika walipoagizwa walipata gari dogo aina ya Lexus likivutwa kutoka majini na gari la polisi.

Lilipofikishwa nchi kavu, alitoka ndani ya gari lao mbio kuenda kuona majeruhi akamuacha muuguzi akisaidiana na askari kutoa machela garini. Alipofika alipata aliyekuwa dereva akiwa amenyongwa kwa usukani, kisha aliyekuwa kando yake chuma ikampitia kifuani hadi moyoni. Alifungua mlango wa nyuma hapo ndipo alipomuona Labibu.

"Doc, do you think she'll survive?!" Muuguzi alimuuliza baada ya kuona hali ya Labibu, "she's in a critical condition and the two are already dead."

"Labda kwa neema ya Maulana," alimjibu lakini akiwa mwenyewe na mashaka kwa maneno yake.

Waliwachukua majeruhi kwa haraka na kuondoka, walipofika hospitali Labibu alilazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na kuwekwa kwenye mtambo wa kupumua.

Mwezi mzima ulipita akiwa pale hali yake si ya kusema, kila asubuhi akifika pale kumwangalia mgonjwa wake, sasa ilikuwa siku ya tatu kutoka alipopata nafuu.

"Daktari, tafadhali nieleze, sikumbuki chochote," Labibu alimgusa tena daktari, "na wazazi wangu je!"

Dk. Jack aliinua kichwa akamwangalia, akaona machozi yanamlengalenga machoni.

"Sir! Are they safe?! Please tell me!" Labibu alimuomba daktari akimuangukia miguuni.

"Maisha ni kama ukungu ambao jua la mauti lichomozapo hayana budi kuondoka," daktari alimwambia akimuinua kisha akamkumbatia, "leo ndiyo siku watakayozikwa. Nimekufahamisha lakini sitakuruhusu uondoke kwa sababu siha yako si njema. Nimefurahi kukuona katika hali hii."

"Lakini daktari, mngeniruhusu masaa mawili niende niwape mkono wa buriani kisha nitarejea," Labibu alimsihi akiufikia mkono wake.

"Ningependa, lakini sina u..."

"Basi nitaenda mwenyewe," Labibu alimkatiza akatoa guo la hospitali na kuanza kutoka.

"Sawa, nitakupeleka kwa gari langu, lakini itakuwa heri tukirudi pamoja."

Walienda hadi maegeshoni wakaingia garini na kuondoka, safari ilikuwa na kimya kirefu. Kwa mara ya kwanza Labibu aliinua uso akamwangalia mwenzake usoni, alionekana mwenye umri wa miaka kama ishirini na tisa hivi.

"Uko sawa au..." Daktari alimuuliza.

"Ndiyo, asante."

"Shukrani ya nini!"

"Kwa kuniangalia kama dadako mdogo kutokea hospitalini."

DK. Jack alicheka kwa maneno ya mwenzake, naye Labibu akatabasamu. Waliendelea na safari kwa masaa manne kabla hawajatia nanga. Walishuka kwa pamoja, Labibu akamkumbatia na kumbusu kwa haraka kisha akaondoka mbio kuelekea palipokuwa na makusanyiko.

Alipofika ndiyo wakati walikuwa wanamaliza kuwafukia wavyele wake, ukemi ulitaka kumtoka akazuia kwa kufunika kinywa akaachia machozi yamtoke.

"Usilie, hii ni njia ya wote," alisikia sauti nyuma yake, alipogeuka na kumuona Shomari alimkumbatia, "nitakuwa nawe kwa kila hali."

Walipogeuka kuanza kuondoka, Labibu alimuona Dk. Jack akija upande wao, wakaenda kukutana na kufahamiana.

"Mshahara wa dhambi ni mauti," Labibu alisikia sauti nyuma yake ikidai.

"Kwa nini watu wakawafikiria wenzao vibaya!" Labibu aliuliza akifuta machozi.

Kabla hajajibiwa, waliona wanahabari kama watano hivi mbele yao wakiwajia kwa kasi, Shomari akawaangalia wenzake kwa mshangao. Wanahabari walifika na kuanza kuuliza maswali moja kwa moja.

"Dada, unaweza ukatuelezea kilichotokea," mwanahabari wa kwanza alianza.

"Nasikia kwamba dereva aliona vizuu barabarani ndipo akapoteza mwelekeo na kutumbukia ndani ya daraja, ni kweli!" Wa pili aliuliza.

"Wakati huu wote umekuwa wapi?."

"Unaweza ukafanya chochote kuzuia ajali nyingine kama hiyo kutokea."

"Una nini cha kuambia vijana wenzako?."

Labibu alionekana kusinyikwa na maswali ya waliomzunguka lakini hakuwa na wa kumsaidia kuwaepuka, alimuona mmoja wa wanahabari akianguka akashtuka.

"You are committing an offence," aliyeangushwa aliboboja kimombo alijizoazoa kutoka chini.

"Mlikuwa wapi wakati huu wote ndo mlete maswali ya upuzi matangani," Shomari aliwauliza kwa pamoja kwa sauti ya kughadhabika akaanza kuwaondoa barabarani, waliondoka wote watatu kwa pamoja.

Baada ya kutembea hatua kadha, Shomari alimgeukia Jack na kumpa mtazamo wa jicho la kumfukuza.

"Namtaka, bado yuko kwa matibabu," daktari alijitetea.

"Dear, utaenda nae au...," Shomari alimuuliza Labibu wake.

Aliyeulizwa alitikisa kichwa, Jack alitoa stakabadhi zake akamkabidhi na kuondoka bila hata kuwaaga. Alirudi hadi garini akaondoka. Wawili hao walisimama kwa muda wakiongea kisha nao wakaenda zao.

***

Chini ya mwembe alipokuwa amepumuzika, aliyaangalia yale mazingira yakampa mvuto kwa kiasi kikubwa. Kile chumba cha Bi. Bela kilikuwa kimezingirwa na miti ya matunda ya kila aina. Kilikuwa kijumba cha msonge kilichojengwa kikajengeka, kilisimama kama malkia katikati ya walinzi wake katikati ya ile miti.

Shomari alimjia kwa utaratibu, alijaribu kusoma mawazo yake bila mafanikio.

"Maisha yanakupeleka vipi?," Shomari alimuuliza kwa ukarimu.

"Ni mazuri, na pia yamenifunza mengi," Labibu alimjibu akimgeukia.

Sura yake ilijaa tabasamu lililomvutia zaidi mwenzake. Shomari kwa upande wake alijua lile jibu lilikuwa la kufunika ugumu aliokuwa anapitia, macho ya mwenzake yalimchunguza. Yale maisha magumu Shomari alikuwa ameyazoea kwa sababu maisha yayo hayo ndiyo yaliyomlea mpaka akafika alivyokuwa.

"Jibu lako ni la kunikinai," Shomari alimpinga, "ulikuwa ushazoea maisha ya kustarehe, kupangia mambo ya juma lijalo leo, sisi hapa hata hatujui kama kesho tutapata cha kutia kinywani. Sisi kulala na kuamka ni kwa neema ya Maulana."

Labibu alicheka kwa maneno ya mwenzake, "ni kweli usemayo, ila sikupata kustarehe hata siku moja kama hapa. Siku zote baba alionekana mwenye shughuli hata akasahau penzi la familia."

"Nimefurahi kusikia hayo mpenzi," Shomari alimkumbatia, "hata hivyo, la mama likikosa la mbwa huamba."

Wote walicheka kwa pamoja, zilikuwa saa nane wakiwa wwmetoka kondeni na hawajatia chochote kinywani ndipo Shomari alipomuona ameketi pekee yake akaamua kuwa mshirika wake kumuondolea mazonge.

Baada ya kusikia yale kutoka kwa mwenzake, hata mtazamo wake juu yake ulibadilika.

"Nambie chochote kuhusu penzi mwenzangu," Labibu alianza.

"Unamaanisha nini!"

"Penzi ni nini au unaweza ukalifananisha na kitu kipi?."

"Penzi ni kama majani, popote hujiotea. Mapenzi hustahimili kiangazi kushinda m'mea mwingine wowote, kiangazi kikizidia hunyauka lakini hata baadae likipata mnyunyizi, penzi huchipuka tena na kuchana kama ua la bondeni."

"Hayo uliyatoa wapi!" Labibu alimuuliza alimuuliza akimwangalia kwa haya.

"Nilifunzwa na bibi," Shomari alimjibu akicheka, "nawe utaniambia nini kuhusu penzi."

"Penzi ni kama mawimbi ya bahari, huwa na nguvu kuliko kitu kingine chochote hapa du..."

"Nawaona katika anga nyingine," Labibu alikatizwa kwa sauti iliyotoka nyuma yao.

"Ah! Mama, kumaanisha umekuwa hapa ukitusikiliza," Shomari alimgeukia mamake.

"Ndiyo mwanangu, 'mi nimekuwa papa hapa, sasa ukaona umuhimu wa kuishi na bibi."

"Ndiyo."

"Na binti je?," Bi. Bela alimgeukia Labibu, "ulipata kumuona bibi yako?!"

"Hapana," alimjibu kwa haraka.

Wote walikaa kimya, Labibu alikuwa akitupa juu embe lililokuwa mikononi na kukama, naye Shomari alikuwa amezamisha kichwa mikononi kama aliyekuwa na mazonge.

"Nataka kuwaona wajukuu wanting kabla sijaaga dunia," mamake alivunja kimya.

Labibu na mwenzake waliangaliana kisha kwa pamoja wakamangalia mnenaji, Labibu moyoni alijua Bi. Bela anamtafutia mwanawe mke kitu kilichokuwa kikitokea kwa nadra sana wakati huo. Maneno ya Bi. Bela alikuwa anakusudia kumchokoza mwanawe.

"Huyu ni mjalaana," maneno aliyosikia siku ya mazishi ya wazazi wake yalimpita akilini, "atakooleka atakiwa amepeleka majanga yake."

"Lakini ma..."

"Hakuna haja ya lakini, binti yangu mwenyewe ushavunja ungo nikuonavyo," mamake Shomari alimpinga Labibu, "wakati wetu, hakuna mtoto ambaye angeweza kuweka neno mbele ya wazazi wake."

"Basi baada yetu kuwa maharusi, zawadi ipi ya kwanza utakayotupa?," Shomari alimuuliza.

"Kwanza kabisa tutahamia katika majengo ya marehemu Bw. Nadama, mali kwa sasa inaharibika bure."

Labibu alimwangalia mamake Shomari kwa mshangao, akajua mara moja nia yake haikuwa ndoa kati yao ila kujipatia mali ambayo ingeitwa kwa jina la mwanawe baada yao kuwa mke na mume.

****

Bw. Siga alivuta nje droo akatoa faili mbili za rangi ya manjano na kuziweka juu ya meza, akaenda upande wa pili wa ofisi akafungua kabati na kutoa stakabadhi zake.

Bw. Vura alikaa akimwangalia kwa mshangao; Bw. Siga alirudi na makaratasi akaweka juu ya meza, akafungua faili alizokuwa ametoa kwa mtoto wa meza na kuanza kuzipekuapekua, aliangalia kila karatasi kwa makini.

"Unafanya nini?," Bw. Vura alimuuliza baada ya kushindwa kuvumilia.

Aliyeulizwa alisitisha shughuli yake akampa mtazamo wa shaka, kisha akaendelea. Alitoa karatasi moja iliyoandikwa MWANGAZA HOLDINGS, akazifunga na kurudisha ndani ya droo.

"Unafanya nini?," mwenzake alimuuliza kwa mara nyingine sauti yake ikiwa na chembechembe za hasira.

"Napanga ofisi tayari kuondoka," Bw. Siga alimjibu, alionekana mwenye mawazo.

"Lakini nilishakwambia kwamba mambo yako nitayashughulikia."

"Semi ni tofauti na vitendo," Bw. Siga alitoa kicheko cha kumdhalilisha mwenzake, "nilikwambia mapema tushughilikie madeni madogomadogo ukapuuza."

"Sikupuuza mwenzangu, lakini pia tunaenda na hali ya uchumi..."

"Kampuni nyingi tulizokuwa tunafanya nazo kazi zishatupa kisogo, zingine zikidai miradi yetu ni ya kiwango cha chini na nyingine zikilalama kuhusu wakati."

Kwa sasa tuna partners wangapi?."

"Ni kampuni moja tu, JDP AGENCIES, na hata wao naona wakikata daraja kwa sababu vifaa tulivyochukua mwaka jana hatujalipia."

"Usijali," Bw. Vura alimwambia, "tutapata wanabiashara wengine."

"Tutapata vipi ikiwa tuna nakisi ya milioni themanini, Lulu Saccos ambao hutupa mkopo jana walipiga simu wakidai."

Bw. Vura mawazo yalimzunguka kichwani, akakumbuka alivyokuwa mbadhirifu akatumia milioni sabakununua gari la kifahari, alionywa na meneja wake kuhusu utumizi wake mbaya wa fedha lakini akapuuza. Alitumia milioni nyingine kumi na mbili kustarehe na mkewe nchini Ufaransa kwa mwezi mmoja, akifanya haya yote wafanyakazi walikuwa wanakatwa elfu mbili kila mmoja wakiambiwa hizo ni pesa za dharura.

"Swala hilo lisikutie shaka ndugu yangu."

"Lisinitie shaka! Miezi sita sasa sijalipwa."

"Nita...," Bw. Vura alikata maneno yake alipoona mwenzake anafungua mlango na kuondoka, aliinuka kitini akaanza kumfuata akimsihi asiondoke. Alijua kumpoteza ni kama kuporomosha kampani lake kitu ambacho hakutaka kitokee. Mwenzake alipuuza maneno yake akaingia garini na kuondoka.

Bw. Vura alibaki pale akifikiri ni nani kati ya wafanyakazi wake anaweza kuchukua nafasi ya Bw. Siga akakosa, aliingia garini naye akaondoka bila hata kuwaaga.

"Nitaifanya kazi hiyo mwenyewe," alijiambia akifuta jasho.

Masaa yalisonga, majuma yakaunga miezi akibambanya pale kwake kama meneja lakini baada ya miezi sita biashara iliporomoka. Hili likitokea kwa sababu ya ukosefu wa uongozi dhabiti, raslimali na ukosefu wa wateja. Baada ya kuporomoka kwa biashara alitoweka hata asijulikane alikoingia. Palipokuwa na kampuni kubwa ya ujenzi palibakia kibao mtini kilichokuwa na ujumbe WHAT IS GOT BY WICKEDNESS FLY AND LEAVES THE OWNER FRUSTRATED.

****

Alipofika kidato cha juu cha mlango wa kanisa, aligeuka na kuangalia waliokuwa nyuma yake kwa masikitiko. Shaka ilimjaa moyoni kwa kile alichokusudia kufanya, waliokuwa nyuma yake walifurahia sherehe.

"Siwezi nikawa mtumwa wa mamake Shomari," Labibu alijiambia kwa sauti ya chini, "i can't ...but how will Shomari think of me!"

Aligeuka na kuanza mwendo kuingia kanisani, rinda lilifagia chini kama la malkia, maua yakatua juu yake kutoka kila upande, alipomuona bwana harusi madhebahuni, moyo ulimdunda kwa nguvu.

Kila jicho pale kanisani lilimwangalia mgeni ambaye alikuwa anatarajiwa. Wengine walibana vinywa kwa mikono yao kwa sababu ya urembo wake.

"Amerembeka kweli," alisikia sauti ikimsemea, "natamani mwanangu ndiye angemuoa, na wakae maisha marefu."

"Kwanza nasikia mavazi yalitoka nchini Tanzania, viatu nchini Kenya, mikufu, herini na vipodozi havijatajwa," alisikia sauti nyingine, "mwangalie binti wa watu analia."

Labibu alishtuka akafuta machozi haraka, alipoangalia upande wa kulia mbele ya umati, alimuona Bi. Bela, alionekana mwenye furaha kuliko hadhira nzima.

Alimnong'onezea jirani yake maskioni, wakageuka na kumtazama Bi. Harusi na kumtolea tabasamu la heri, mwenyewe moyoni hakuwa amefikia uamuzi.

"Binti mzuri kama huyu Shomari 'kamtoa wapi! Anaonekana 'kaumbwa kwa mavumbi ya nyota," alisikia sauti ikidai.

"Hata 'mi sijui, ila nasikia ni mtoto wa marehemu Bw. Nadama na Bi. Tabasuri. Nasikia ndiye akagharamikia hivi vyote."

Labibu alienda akasimama kando ya mtu ambaye dakika chache baadae angeitwa mumewe, alimwangalia Shomari akaona anatabasamu, lakini mwenzake hakumsoma kwa sababu ya ushungi uliokuwa usoni.

Mpatanishi aliyekuwa anawaunganisha maharusi aliinuka tayari kutimiza wajibu wake.

"Uko tayari kumtua Labibu kama mkeo kwa shida na raha?," Alimuuliza Shomari.

"Ndiyo, nipo tayari," Bw. Harusi alikubali akimvika pete kidoleni.

Labibu alitoa ushungi usoni, Shomari akaona alama ya michirizi ya machozi, akadhania labda mwenzake alilia machozi ya furaha. Umati ulipasua hewa kwa makofi, vifijo na nderemo baada ya bibi harusi kuvikwa pete.

"Uko tayari kuwa na Bw. Shomari mpaka kifo kiwatenganishe," mpatanishi alimgeukia bibi harusi.

Kimya kilitanda, dakika mbili zilipita bila jibu kutoka kwa bibi harusi, mpatanishi akarudia tena maneno yake bila kukata tamaa. Kimya kilizidi wengine wakadhania labda ni kwa sababu ya uoga, michirizi ya machozi ilimtoka Labibu, pete iliyokuwa mkononi ikaanguka, kijasho kikamtoka bwana harusi akafuta kwa kitambaa.

"Narudia tena, uko tayari ku..."

"Hapana!" Mpatanishi alikatizwa kwa sauti ya kelele iliyomtoka bibi harusi, akasonga nyuma kwa uoga.

Alivuta rinda lake akaanza mbio kutoka kanisani.

"Ah! Makubwa haya," alisikia hadhira ikimaka, "amemtenda mtoto wa watu kweli."

Shomari alibaki madhebahuni kinywa wazi, hakuamini macho yake, lakini mwenzake alipofaulu kutoka nje ya kanisa aliabiri taksi iliyokuwa karibu.

"Wapi?!" Dereva alimuuliza kwa mshangao baada ya kuona rinda lake.

"Matopeni street," Labibu alimjibu bila hata kufikiri.

Akiwa garini, alifaulu kutoa rinda la harusi akavalia suruali ndefu na t- shirt nyeupe iliyoandikwa kifuani "Depressed in love" . Alianza kujutia alichokuwa amefanya lakini akajiona amefanya uamuzi murwa, hakuwa tayari kufanywa mtumwa na yeyote.

Alianza kukumbuka chanzo cha kile alichokuwa amemtenda mwenzake.

Siku ya kwanza kufika kwa Bi. Bela, alijua tabia zake.

Walipofika walikaribishwa kwa furaha na mwanamke yule, alipomwangalia usoni alisoma tabasamu lake. Ilikuwa tabasamu ya kinafiki, dakika chache baada ya kufika kwao alimvuta mwanawe chemba.

"Unafikiri unafanya nini? Huyu msichana ukamleta hapa kwa nini!" Alimsikia Bi. Bela akimkaripia mwanawe.

"Nimemleta tuis..."

"Utaniletea majanga hapa nyumbani, unajua alipoteza wazazi wake kwa njia ya kutatanisha. Hayo mazingaobwe umeyaleta hapa!"

"But mu..."

Aliposikia maneno ya mwenyeji wake alitoka nje polepole, akafuta machozi na kuanza kuondoka, ilikuwa saa tatu za usiku.

"Usiondoke," Shomari alimsihi akimfikia, "it's already late."

"Hakuna haja nisababishe ugomvi kati yenu," alimwambia akijinasua na kuondoka.

Majuma yalipita kila mara Shomari akimshawishi warudi nyumbani kwao waishi pamoja, baada ya mvutano wa muda alikubali shingo upande akifikiri labda Bi. Bela atabadili mtazamo wake kumuhusu.

Mambo yalijirudia mwezi mmoja baada ya kupangwa kwa harusi yao, ambaye angekuwa ma'mkwewe alianza kumchunga kama kondoo, mwenyewe hakujishughulisha naye sana.

Kama matayarisho ya maisha mapya, aliandika hundi ya millioni tano ujenzi wa nyumba ambayo wangeishi ukaanza.

"Unafaa ubadili tabia zako kwa sababu kuanzia kesho utakuwa mke mtu," alikumbuka alivyojibiwa usiku huo wa kuamkia harusi.

Bi. Bela alikuwa ashachoma baadhi ya nguo zake juma moja kabla akidai atakuwa na jicho la nje. Hayo yote yakitokea hakumwambia mpenziwe kwa sababu alijua hatasikilozwa, hayo ndiyo ilikuwa sababu kuu ya kile alichotenda.

****

Labibu aliangalia kitabu kilichokuwa mbele yake kwa chuki, akainuka na kuelekea ukingoni mwa ziwa kisha akapumzika chini ya mnazi uliokuwa umemea kando.

Alianza kupekuapekua kurasa za kile kitabu kwa utaratibu, alipofikia ukurasa mmoja alishtuka, kilichomshitua ni mwandiko wa laini kama tatu hivi zilizoandikwa kwa mlazo.

...hata kama univunja moyo, nikalala gizani, machozi yalinijaa usoni yakitiririka kutoka moyoni. Sitaondoka kando yako, nikiwa hai au mfu, utasalia kuwa habubana rafiki ya gu.

Ujumbe ule ulimshitua hata zaidi, alishindwa namna Shomari alivyopata daftari lake na kuandika kile kifungu kilichomchoma mpaka moyoni akahisi amepata jeraha.

"Kwa nini akayaandika haya?!," Alijiuliza akitikisa kichwa, "tena alijua vipi janga hilo litatokea?!."

Kwa hasira alirarua ule ukurasa na kuutupa majini.

"Kwa nini umerarua," sauti ilitokea nyuma yake, "nafikiri hata labda hu..."

"And how dare you ask me such silly question you poor thing," Labibu alifoka kwa hasira.

"Sorry, I didn't intend to offend you," yule mvulana alimwambia akisonga nyuma kwa uoga.

"Am sorry too," Labibu alitoa radhi, "ndoo tupumuzike."

Yule mvulana alienda akaketi kando yake, wote wakaangaliana karatasi lililotupwa ziwani lilivyotoswa kila upande na mawimbi hafifu ya ziwani.

Labibu alifunga daftari lililokuwa mbele yake na kumtazama yule kijana, alionekana aliyekuwa na neno la kumwambia lakini akahisi uoga.

"Naitwa Jaqy, ila wengine huniita JQ," yule mvulana alijitambulisha kwa mwenzake.

"Nami naitwa Labibu."

Japo ilikuwa mara ya kwanza kuonana, mvuto ulikuwa ushajengeka kati yao kwa kile kipindi kifupi.

"Nilikuona hapa pekee yako nikaja kukuondolea upweke, tena mahali hapa ni hatari," JQ alimwambia.

"Nami ni mtu hatari, ni kama mjalaana wa kukimbiwa na ulimwengu," Labibu alimumwagia joto la moyo wake.

"Usiseme maneno ha..."

"Nitafaulu kukichapisha?!"

"Wow! You are a bright girl," JQ alimaka baada ya kukabidhiwa lile daftari na mwenzake, "and what drove you to write such a manuscript?!"

Labibu pasipo kupoteza hata nukta, alianza kumsimulia kilichokuwa kimemfanya mpaka kuandika ule mswada. Mada ya mswada na umri wa mwandishi vilivyomshitua sana JQ, mada yake ilikuwa CHOZI LA UNYONGE.

"I think sometimes life is always unfair for it turns out how we don't expect it to," Labibu alimwambia katikati ya kicheko cha uchungu, "tena, kwa nini Mola akaruhusu mabaya kuwatendekea wema."

"Kwa nini mara nyingi tukamtupia Maulana lawama...," JQ alicheka kumtuliza mwenzake, "haya mambo hutendwa na insi, tena walio karibu yetu, na hata wakati mwingine ujinga wetu wenyewe ukatuingiza pabaya, kisha lawama tukamrudishia asiyestahili. Ama hujui kwamba heri rafiki mkweli kuliko ndugu mnafiki."

Labibu alitabasamu kwa maneno ya mgeni wake ambaye hata hakujua asili yake, akamkumbatia akifuta machozi yaliyokuwa machoni. JQ kwa upande wake alihisi kitu kigeni kikiwa kimemtendekea maishani.

"You are my first born boy child," Labibu alimwambia, "now tell me am you favourite girl."

"Anyway am not a lover boy because I know, love is for the strong who are ready to be broken hearted, whose devotions and emotions speak louder than words, and who are always looking for affection rather than perfection in a relationship, but for me am too weak for that."

"Nishasikia Kenya kwa muda, nafikiri ndiyo nchi nzuri zaidi duniani," Labibu alimwambia baada ya kuona kimapenzi hawatafika mbali.

"Ni kweli, lakini kuna mnyama anaitwa ufisadi anawatesa wananchi na walio uongozini wameshindwa kukabiliana naye. Kila baada ya miaka kampeni zivumapo ufisadi huwa ajenda ya kwanza katika kinywa cha kila mwanasiasa, lakini ni kama maneno ya kupita na upepo."

"Utanipeleka huko habuba wangu!"

"Nitakubali ombi lako ikiwa kuanzia sasa utakubali nikuite Christabel."

Wote walicheka, JQ alifikiri maneno ya mwenzake ni mzaha, lakini msemaji alikuwa ameyatilia manani. Labibu alimuongoza mpaka nyumbani kwa wazazi wake, akajitayarisha tayari kwa safari.

"Heri tungejipanga kwa juma moja mpenzi!"

"Nina kila kitu habuba wangu," Labibu alimwambia akimpiga vikofi mgongoni, "hatuna haja ya kuchelewa Gunga, kama pesa zi..."

"Pesa si kila kitu katika maisha ya mwanadamu," JQ alimkatiza, "nakumbuka ipo siku mwalimu alituletea mada hii tujadili katika mjadala PESA NDICHO CHANZO CHA UOVU DUNIANI."

Labibu alimwangalia akamtolea tabasamu la heri, "i also remember viewing anyother girl's WhatsApp discription, it said life is laughing, loving, have fun and sleep. It really motivated me, you don't have to depend on money."

***MWISHO***


next chapter
Load failed, please RETRY

Bald kommt ein neues Kapitel Schreiben Sie eine Rezension

Wöchentlicher Energiestatus

Rank -- Power- Rangliste
Stone -- Power- Stein

Stapelfreischaltung von Kapiteln

Inhaltsverzeichnis

Anzeigeoptionen

Hintergrund

Schriftart

Größe

Kapitel-Kommentare

Schreiben Sie eine Rezension Lese-Status: C12
Fehler beim Posten. Bitte versuchen Sie es erneut
  • Qualität des Schreibens
  • Veröffentlichungsstabilität
  • Geschichtenentwicklung
  • Charakter-Design
  • Welthintergrund

Die Gesamtpunktzahl 0.0

Rezension erfolgreich gepostet! Lesen Sie mehr Rezensionen
Stimmen Sie mit Powerstein ab
Rank NR.-- Macht-Rangliste
Stone -- Power-Stein
Unangemessene Inhalte melden
error Tipp

Missbrauch melden

Kommentare zu Absätzen

Einloggen